Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu
Tanzania Bara, Azam FC, kinatarajiwa kutua leo nchini kutokea Lubumbashi, DR Congo
kikiwa na matumaini makubwa ya kuanza vyema michuano ya kimataifa baada kuyafanyia
kazi mambo kadhaa.
Azam iliondoka nchini mapema, Januari 27,
mwaka huu kwa ajili ya kuweka kambi na kushiriki michuano maalum baada ya
kupata mualiko kutoka kwa Klabu ya TP Mazembe.
Timu hiyo ikiwa nchini humo, iliendelea na mazoezi
yake na kucheza michezo na timu tofauti ikiwemo TP Mazembe, Don Bosco na Zesco
ya nchini Zambia, kwa ajili ya maandalizi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Itacheza
na El Merreikh ya Sudan Februari 15.
Meneja wa
timu hiyo, Jemedari Saidi, alisema timu hiyo ina matumaini makubwa ya kuanza
vyema michuano yake kutokana na maandalizi waliyofanya.
“Timu inatarajiwa kutua kesho Jumatano baada
ya kumaliza michuano yake ambayo ilialikwa nchini Kongo na mwalimu Joseph Omog
ameitumia vyema kuhakikisha anakuwa na kikosi bora zaidi kwa ajili ya michuano
ya kimataifa,” alisema Jemedari.
0 COMMENTS:
Post a Comment