Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Azam FC wamekubali kuipisha Yanga kileleni.
Azam FC imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi, Pwani.
Sare hiyo ya bila mabao, inaifanya Azam FC kufikisha pointi 26 wakati Yanga ambayo imeibuka na ushindi dhidi ya Prisons inafikisha pointi 28.
Azam FC ndiyo inaongoza kwa kuwa na pointi 25 sawa na Yanga lakini tofauti ilikuwa ni mabao ya kufunga na kufungwa.
Katika kipindi cha kwanza dakika 15 za kwanza, Azam FC ilishambulia zaidi, lakini washambuliaji wake John Bocco na Kipre Tchetche hawakuwa makini.
Kipindi cha pili, mambo yalibadilika na Ruvu Shooting kutawala huku wakionekana kuwasumbua Azam FC, hata hivyo nao hawakuwa makini kumalizia nafasi walizozipata.







0 COMMENTS:
Post a Comment