February 19, 2015


MPIRA UMEKWISHA
Dk 90+4
Dk 90+3 Hamis Mainge anaingia kuchukuana nafasi ya Mpalile kwa Prisons
Dk 90+2 Yanga wanaendelea kucheza fupifupi
Dk 90+1Yanga wanacheza pasi fupifupi
Dk 88 Jeremiah Juma anapiga shuti akiwa katika nafasi nzuri lakini Barthez anaokoa vizuri kabisa.

Dk 81 hadi 87, mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja huku mipira mingi inayofika langoni inakuwa laini. Yanga wanaonekana kucheza zaidi pasi fupifupi kuonyesha wameridhika na mabao yao matatu.

Dk 80, Fredy Chudu analambwa kadi ya njano baada ya kumkanyaga kwa makusudi Niyonzima (alistahili kadi nyekundu).
DK 78 Yanga wanamtoa Yondani na nafasi yake inachukuliwa na Rahab Zahir

Dk 75, krosi safi ya Juma Abdul inatua kichwani mwa Msuva, peke yake anashindwa kulenga lango

Dk 74, Ngassa anashindwa kufunga akiwa hatua chache kutoka hatua chache katika lango la Prisons
Dk 69 Yanga wanafanya shambulizi kali, ndani ya eneo la 18 lakini Prisons wanaokoa 
Dk 66, Yanga wanamtoa Coutinho na nafasi yake inachukuliwa na Danny Mrwanda

Dk 65, Hassan Omar anaingia kwa upande wa Prisons

Dk 64, Jeremiah Juma anampa pasi nzuri Mwakalobo lakini anashindwa kufunga 
GOOOOOOOOO Dk 62, Msuva anawatoroka mabeki wa Prisons na kupiga kichwa safi akiunganisha mpira wa kona wa Coutinho na kuipa Yanga bao la tatu.

Dk 54, Yanga inamtoa Twite mwenye kadi ya njano na nafasi yake inachukuliwa na Salum Telela

KUTOKA MABATINI (JKT RUVU VS AZAM FC): HADI SASA SARE YA BILA KUFUNGANA, DAKIKA YA 78

Dk 52, kipa Prisons anafanya kazi ya ziada na kuokoa mpira miguuni mwa Ngassa
Dk 49, Jacob Mwakalobo anampiga kanzu kipa wa Yanga, lakini mpira unamzidi kasi na kutoka nje.
Dk 47, Twite anapiga shuti kali lakini linatoka nje pembeni ya lango la Prisons

Dk 47 Prisons nusura wajifunge lakini kipa anaokoa baada ya beki kupiga kwenye lango lake
MAPUMZIKODk 45+1 Twite anapiga shuti kali akiwa ndani ya 18 lakini anapaishaa puuuu.

Dk 44, Tambwe anapoteza nafasi tena baada ya kupewa nafasi nzuri na Msuva.
Dk 32 hadi 35 timu zote zaidi zinacheza katikati ya uwanja

Dk 30 Amir Juma anapiga shuti kali baada ya mabeki wa Yanga kuchanganyana lakini Barthez tena anaokoa uzuuuri.

Dk 37, Barthez anaokoa mkwaju mkali wa faulo

Dk 36, Twite analambwa kadi ya njano
Dk 33, mpira wa adhabu wa Prisons, Barthez anafanya kazi ya ziada kuokoa
Dk 31, Yanga wanapata nafasi nzuri lakini Msuva na Ngassa wanashindwa kuwa makini

Dk 28, Mwamuzi anamlamba Amir Juma Kadi ya njano kwa kumpiga teke Twite
Dk 26, Juma Abdul anapiga krosi nzuri baada ya kupokea pasi ya Coutinho, hata hivyo kipawa Prisons anajitokeza na kudaka

Dk 17, krosi nzuri ya Juma abdul, Tambwe anapotea na kupiga kichwa butu

GOOOOOOOOOOO  Dk 11, Coutingo anaifungia Yanga kupata bao la pili kwa shuti kali baada ya kipa kupangua shuti kali la Amissi Tambwe.

Dk 10 Jeremiah Juma anapiga shuti ndani ya eneo la hatari lakini Ally Mustapha anaokoa vizuri.


Dk 9, Yanga wanapata nafasi baada ya krosi nzuri ya Juma Abdul, lakini Haruna Niyonzima anapiga shuti mtoto.
GOOOOOOOOO DK 3, Msuva anaifungia Yanga bao la kwanza baada ya kuruka juu na kuunganisha mpira wa kocna wa Coutinho.

Dk 1, Prisons wanapata mkwaju wa adhabu, wanapiga lakini unaishia mikononi mwa Batrhez.


Mechi imeanza na timu zote zinaonekana kuanza kwa umakini mkubwa zikisomana kwa hofu ya kutofungwa bao la mapema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic