| KIKOSI CHA RUVU SHOOTING |
Msemaji wa
JKT, Masau Bwire amesema mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Azam FC wamepata bahati ya mtende kupata sare.
Azam FC
imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi Kuu
Bara kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi, Pwani.
![]() |
| MASAU BWIRE. |
Masau amesema
kupoteza nafasi nyingi kumechangia wao kuwakosa Azam.
“Tuliwazidi
kila kitu, tulikuwa na uhakika wa kuwashinda. Basi tu tulipoteza nafasi
wenyewe.
“Kwa kweli
Azam FC wanapaswa kushukuru kwa kuwa na bahati hiyo,” alisema.
Kwa upande wa
Azam FC, msemaji wao, Jaffar Iddi amesema uwanja mbovu ndiyo ulichangia wao
kutoibuka na ushindi.
“Ilikuwa si
lahisi kucheza katika kiwango chetu kwa kuwa uwanja wa Mabatini ni mbovu sana
na haustahili kabisa kuchezewa.
“Ukiangalia
kwa juu, unaweza kudhani ni uwanja mzuri lakini ni mbaya na una mabonde mengi,”
alisema Jaffar.








0 COMMENTS:
Post a Comment