Klabu ya
Chelsea imetangaza kuwasimamisha mashabiki wake watatu kuingia kwenye Uwanja wa
Stmaford Bridge, London.
Chelsea
imewazuia mashabiki hao baada ya kubainika walishiriki katika kitendo cha
ubaguzi dhidi ya mtu mmoja mweusi jijini Paris, Ufaransa.
Mashabiki hao
walimsukuma mtu huyo wakimzuia kuingia kwenye treni wakati wakiwa wanakwenda
kuangalia mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya PSG.
Mtu huyo
alijaribu kuingia kwenye treni lakini walimsukuma huku wakiimba “Sisi ni
wabagusi, sisi ni wabaguzi”.
![]() |
| MTU ALIYEZUIWA KUINGIA KWENYE TRENI NA MASHABIKI HAO AKIWA NJE YA TRENI BAADA YA KUSUKUMWA... |
Kitendo hicho
kimeonekana kwenye picha ya video na kuwaudhi wadau wengi wa michezo na
wamekuwa wakisisitiza wachukuliwe hatua.
Chelsea
imetangaza kuwasimamisha kuhudhuria kwenye uwanja wake na uchunguzi unaendelea
kufanyika. Iwapo watabainika kushiriki moja kwa moja, basi watakungiwa maisha.
BLOG HII
INALAANI VITENDO VYA KIBAGUZI KAMA HIVYO VILIVYOFANYA NA MASHABIKI WA CHELSEA
KUWA NI UPUUZI MKUBWA.









0 COMMENTS:
Post a Comment