Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime, amesema ana imani kikosi chake kitarejea kileleni mwa Ligi Kuu Bara.
Maxime amesema wamekuwa wakiendelea kupambana kurekebisha makosa kadhaa ambayo yamewapelekea kucheza mechi sita bila kushinda.
"Sisi tunajua tunaweza kurekebisha mambo na kurudi katika hali yetu. Bado tunapambana na ikiwezekana turuki kileleni.
"Najua watu watasema ni vigumu, ila sisi tunajua itawezekana kama ambavyo tuliweza awali," alisema.
Mtibwa Sugar imekuwa ikisonga kwa mwendo wa kusua na sasa iko katika nafasi ya tano ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi 13.
Maxime anaamini bado wana nafasi ya kurudi kileleni kwa kuwa bado wana kikosi bora na kinara Azam FC ana pointi 25 tu ambazo ni tofauti ya pointi sita pekee.








0 COMMENTS:
Post a Comment