Pamoja na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0
dhidi ya BDF XI ya Botswana katika mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho
Afrika wikiendi iliyopita, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Mnyarwanda, Haruna
Niyonzima, amesema ana hofi na mchezo wa pili.
Yanga inatarajiwa kurudiana na BDF XI Februari
28 nchini Botswana na itatakiwa kuhakikisha inafanya vizuri katika mechi hiyo ili
iweze kujikatia tiketi ya kusonga mbele kwenye hatua nyingine ya michuano hiyo.
Niyonzima amesema bado
wana kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha wanasonga mbele kwenye mashindano
hayo kutokana na ubora wa wapinzani wao.
“Wito
wangu kwa kocha ni kuhakikisha anaufanyia kazi upungufu wote uliojitokeza katika
mechi yetu ya kwanza ili usije kutusababishia matatizo tutakaporudiana.
“Mabao mawili siyo mengi sana na hivyo tusipojiandaa
vizuri tunaweza tukajikuta tunatupwa nje, tunatakiwa kwenda kwa nia ya kushinda
au kupata sare yoyote,” alisema Niyonzima.
Katika mechi dhidi ya BDF jijini Dar es Salaam, Niyonzima alicheza katika kiwango kizuri na kuwa mwiba kwa safu ya kiungo na ile ya ulinzi ya Waswana hao.







0 COMMENTS:
Post a Comment