Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesisitiza
hata kama iko ugenini, Simba inalazimisha kushinda dhidi ya Kagera Sugar.
Kocha huyo Mserbia amesema mechi hiyo ya
wikiendi itakuwa ngumu kwao kutokana na ubora, lakini suala la ushindi ni
muhimu.
“Tunajua Kagera ni timu nzuri, lakini katika
ligi hii kumbuka hakuna timu dhaifu.
“Ila kuna timu kongwe na timu imara zaidi. Sisi tunachoangalia
ni kufanya vizuri na kushinda.
“Tutaanza safari ya kwenda Kagera tukiwa na
lengo moja tu, kushinda mechi na kurudi na pointi tatu,” alisisitiza MSerbia huyo.
Simba imekuwa ikiendelea kujifua kwenye Uwanja
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment