Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm
ameendelea kulifanyia kazi kwa vitendo suala la wachezaji wake kupoteza nafasi
nyingi.
Kocha huyo raia wa Uholanzi, amekuwa
akiwaonyesha wachezaji wake wanastahili vipi kupiga mipira.
Pluijm amesema iwapo watakuwa na uwezo wa
kutumia nafasi, basi watafika mbali.
“Nafasi tunazotengeneza ni nyingi sana. Hivyo tunastahili
kuzitumia kwa faida yetu.,
“Unapokosa nafasi kwa asilimia zaidi ya hamsini,
maana yake hauko makini. Sasa lazima tuwe makini na kuzitumia,” alisema Pluijm.
Mara kadhaa, Mholanzi huyo alikuwa akiwaonyesha
wachezaji wake namna ya upigaji sahihi na kufunga.
Pluijm ambaye amewahi kuidakia timu ya taifa ya
Uholanzi, aliwataka wachezaji waongeze umakini.
0 COMMENTS:
Post a Comment