March 22, 2015







MPIRA UMEKWISHA
DK 88 baba Ubaya anapewa kadi ya njano kwa madhambi
Dakika za mwisho Simba wanacheza mpira wa pasi zaidi kuonyesha wameridhika na bao tatu huku Ruvu nao wakionyesha kukata tamaa.
Dk 81 Simba wanamtoa Tshabalala na nafasi yake inashukuliwa na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’


Dk 75 Maguri anaifungia Simba bao la tatu baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa baada ya shuti Ndemla aliyewachambua mabeki.
Dk 72, Ruvu wanamtoa Juma Nade na nafasi yake inachukuliwa na Juma Ndindi
Dk 71Singano, akiwa katika nafasi nzuri kabisa, anashindwa kufunga huku kiopa akiwa ameacha wazi sehemu kubwa ya lango.


Dk 69, Simba wanamtoa Okwi na nafasi yake inashukuliwa na Elius Maguri.


GOOOOOOOOO DK 61, Awadhi anawachambua mabeki wa Ruvu na kupiga shuti kali linalomgonga beki na kujaa wavuni.

GOOOOOOOO Dk 60 Ajibu Anafunga vizuri mkwaju wa penalti na kuipa Simba bao.


PENAAAAAAT Dk 58 Awadhi Juma anaagusha katika eneo la 18, mwamuzi anaweka mkwaju wa penalti

DK 55, Tumbo anapata pasi nzuri, nafasi nzuri lakini yeye na lango, nashindwa kufunga.


Kipindi cha pili kinaanza kwa kasi kubwa, Simba kama walivyoanza kipindi cha kwanza. Wanakianza cha pili kwa kasi kubwa wanapeleka mashambulizi mfululizo lakini vilevile wanashindwa kutumia nafasi.


MAPUMZIKO:
Okwi anapiga shuti kali linagonga mwamba na kutoka kurudi uwanjani
Dk 45+3
Dk 44 Okwi analambwa kadi ya njano kwa kushika mpira

Dk 39, Okwi anapi mpira dhaifu wakati unaelekea langoni, mabeki Ruvu wanautoa na kuwa kona
Dk 34, Tumbo anapiga kichwa safi lakini kipa Peter Manyika anadaka kwa ulaini
Dk 29, THIS IS TOO MUCH aisee, Okwi tena akiwa hatua tatu kutoka lango la Ruvu, anapiga kichwa cha kuchumpa kinatoka nje. Eh!
Dk 24, Simba wanapoteza nafasi nyingine baada ya Singano kubaki yeye na kipa tu lakini anampa mikononi.


Dk 21 Yayaha Tumbo anakimbia na kupiga shuti kali linalopaa. Hili ndiyo shambulizi la kwanza la Ruvu Shooting langoni mwa Simba.

Dk 18, Ajibu anazuga kama anatoa pasi, lakini mpira unapaa kidogo.
Dk 11, Simba wanapoteza nafasi nyingine unaweza usiamini, Okwi anapiga kichwa, mpira unamgonga kipa unarudi.
Ndemla akiwa amebaki na anashindwa kufunga na beki anaokoa.
Dk 10, Simba wanapoteza nafasi tena, safari hii akiwa amebaki na kipa baada ya mabeki  kuaguka.

Dk 6 Simba wanapoteza nafasi nyingine baada ya kuteleza na kuanguka na kushindwa kufunga krosi nzuri ya Singano.
Dk 3, Ajibu anapokea krosi safi ya Kessy na kupiga kichwa kinapaa juu

Dk 2 Okwi anaingia kwenye lango la Ruvu lakini kipa anajotokeza na kudaka

Dk 1 Simba wanafanya shambulizi kali lakini mpira unaokolewa na mabeki Ruvu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic