Azam FC imeendelea na mazoezi leo kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga kujiandaa na mechi ya keshokutwa dhidi ya wenyeji wake Coastal Union.
Moja ya kivutio katika mazoezi yao ni meneja wa timu hiyo, Jemedari Said.
Jemedari aliyekuwa kiungo nyota wa Kariakoo Lindi aliungana na wachezaji wa Azam FC kufanya mazoezi.
Wakati akimiliki mpira na kutoa pasi, Jemedari alionekana kama mmoja wa wachezaji wa Azam FC na baadhi ya mashabiki walishangazwa kumuona akiwa fiti.
Wengine walisifia kwamba mameneja wa timu wanapaswa kuwa 'active' kama Jemedari.







0 COMMENTS:
Post a Comment