Huku Ligi
Kuu Bara ikiwa inaendea ukingoni, ushindani unazidi kuongezeka.
Ushindani
unazidi kupamba moto kutokana na timu tatu kubwa za Yanga, Simba na Azam FC
kuzidi kujiongozea pointi baada ya ushindi wa siku mbili.
Yanga
imefanikiwa kujiongezea pointi kwa kuishinda Mgambo Shooting kwa mabao 3-0
kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, jana.
Wakati
Yanga imeshinda jana, Azam FC nayo imeshinda kwenye uwanja huo kwa kuichapa
Coastal Union bao 1-0.
Simba
nao walikuwa Uwanja wa Taifa, Dar, nao wakashinda kwa mabao 3-0 dhidi ya timu
ngumu ya Ruvu Shooting.
Kutokana
na ushindi wa timu zote tatu, Yanga imefikisha pointi 40 na kujichimbia zaidi
kileleni huku Azam ikibaki nafasi
ya pili na pointi 37 na Simba ni ya tatu ikiwa na 32.
Ingawa
Azam FC inabaki mchezo mmoja wa kiporo ili kufikicha mechi 19, si lahisi
kuidharau Simba kwa kuwa iko katika timu tatu zilizovuka pointi 30.
Yanga
ndiyo timu pekee iliyofikisha pointi 40 na Azam iko katikati ya 30, hivyo
kuifanya ligi iwe haitabiriki kwani timu ikiboronga mechi mbili, basi mambo
yanakuwa magumu.
Zaidi
ni Yanga na Azam FC nambao ni mabingwa watetezi wanaoonekana wana nafasi ya
kutwaa ubingwa. Lakini hii haiizuii Simba kuitibulia moja wapo katika nafasi ya
pili na kujikuta ikiangukia katika nafasi ya tatu.
Hali
hiyo inazidi kuongeza presha kwa makocha wa timu zote tatu ambao wanatokea nje
ya Tanzania.







UONGO MTUPU,SHUUUUUUUUUUUUUUUU
ReplyDelete