March 22, 2015


Huku Ligi Kuu Bara ikiwa inaendea ukingoni, ushindani unazidi kuongezeka.

Ushindani unazidi kupamba moto kutokana na timu tatu kubwa za Yanga, Simba na Azam FC kuzidi kujiongozea pointi baada ya ushindi wa siku mbili.

Yanga imefanikiwa kujiongezea pointi kwa kuishinda Mgambo Shooting kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, jana.

Wakati Yanga imeshinda jana, Azam FC nayo imeshinda kwenye uwanja huo kwa kuichapa Coastal Union bao 1-0.

Simba nao walikuwa Uwanja wa Taifa, Dar, nao wakashinda kwa mabao 3-0 dhidi ya timu ngumu ya Ruvu Shooting.

Kutokana na ushindi wa timu zote tatu, Yanga imefikisha pointi 40 na kujichimbia zaidi kileleni huku  Azam ikibaki nafasi ya pili na pointi 37 na Simba ni ya tatu ikiwa na 32.

Ingawa Azam FC inabaki mchezo mmoja wa kiporo ili kufikicha mechi 19, si lahisi kuidharau Simba kwa kuwa iko katika timu tatu zilizovuka pointi 30.

Yanga ndiyo timu pekee iliyofikisha pointi 40 na Azam iko katikati ya 30, hivyo kuifanya ligi iwe haitabiriki kwani timu ikiboronga mechi mbili, basi mambo yanakuwa magumu.

Zaidi ni Yanga na Azam FC nambao ni mabingwa watetezi wanaoonekana wana nafasi ya kutwaa ubingwa. Lakini hii haiizuii Simba kuitibulia moja wapo katika nafasi ya pili na kujikuta ikiangukia katika nafasi ya tatu.


Hali hiyo inazidi kuongeza presha kwa makocha wa timu zote tatu ambao wanatokea nje ya Tanzania.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic