Baada ya juzi Jumamosi
kufanikiwa kuifunga Mgambo JKT mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini
Tanga, sasa vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wamebakiza mchezo mmoja tu ambao ni
sawa na dakika tisini, nje ya Jiji la Dar.
Yanga wamejikusanyia pointi
37 kwa kucheza michezo 18, wamebakiza michezo nane tu ili kuhitimisha ligi hiyo
msimu huu ambayo inatarajiwa kufikia tamati Mei 9, mwaka huu.
Katika michezo hiyo nane,
Yanga itacheza michezo saba mfululizo katika Uwanja wa Taifa jijini Dar ambao
wanautumia kwa michezo yao ya nyumbani huku ule wa mwisho wakilazimika kusafiri
mpaka mkoani Mtwara kupambana na Ndanda FC kwenye Dimba la Nangwanda Sijaona.
Wakati Yanga ikiwa imebakiza
mchezo mmoja ugenini, wapinzani wao wanaowafuatia kwa karibu, Azam nao pia
wamebakiza mchezo mmoja dhidi ya Mtibwa Sugar huku Simba wao wakiwa wamebakiza
michezo miwili ambapo watacheza dhidi ya Kagera na Mbeya City.
Yanga na Azam zina nafasi
kubwa ya kulitwaa kombe hilo endapo tu zitatumia vizuri mechi hizo za nyumbani.







0 COMMENTS:
Post a Comment