Basi la wachezaji wa kikosi cha Fenerbahce limeshambuliwa
na dereva wake kupigwa risasi.
Dereva huyo wa basi lililokuwa limebabe
wachezaji na viongozi 40 alipelekwa hospitali kwa matibabu baada ya kujeruhiwa
usoni.
Wachezaji hao walikuwa wanatoka kucheza katika
moja ya mechi za Ligi kuu Uturuki, dereva huyo aliposhambuliwa.
Mlinzi aliyekuwa ndani ya basi hilo alilazimika
kuwahi kuliendesha basi hilo hadi liliposimama.
Hata hivyo kumekuwa na utata wa risasi
iliyompiga dereva huyo ni kutoka katika bunduki ya aina gani.
Gavana wa eneo la Trabzon, Abdulcelil Oz amesema
dereva amepigwa na risasi lakini wanaendelea kufanya uchunguzi.
0 COMMENTS:
Post a Comment