Kamati
ya Mashindano ya TFF ilikutana jana kupitia maandalizi ya Ligi ya Mabingwa wa
Mikoa (RCL) pamoja na taarifa ya Ligi Daraja la Pili (SDL) iliyomalizika hivi
karibuni.
Katika
matukio ya SDL, Kamati imeipiga faini ya sh. 300,000 timu ya JKT Rwamkoma ya
Mara kwa kusababisha mechi yake dhidi ya AFC ya Arusha kuvurugika. Adhabu hiyo
kwa mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid
jijini Arusha imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(4) ya Ligi Daraja la Pili.
Nao
makocha wa JKT Rwamkoma, Hassan Makame na Kamara Kadede wamepigwa faini ya sh.
200,000 kila mmoja na kufungiwa mechi sita kwa kumshambulia mwamuzi msaidizi
namba moja katika mechi hiyo iliyochezwa Machi 9, 2015.
Wachezaji
Shafii Maganga, Saleh Ali, Ismail Salim na Mussa Senyange wa JKT Rwamkoma ambao
wanatuhumiwa kwa kushambulia mwamuzi kwenye mechi hiyo suala lao linapelekwa
kwenye Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa hatua zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment