Katibu
Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine leo amefungua rasmi semina ya waamuzi vijana
wenye umri wa miaka 12- 17, inayofanyika katika hostel za TFF zilizopo Karume.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mwesigwa amesema semina hiyo ya vijana imejumuisha
vijana 27 kutoka mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaandaa kuwa waamuzi wa
kimataifa baadae.
Vijana
hawa mnaowaona hapa wanatoka katika viuto vya kufundishia waamuzi vijana
nchini, wakikua na kufuata misingi ya kazi baadae watakua waamuzi bor nchini
kwa sababu watakua wameanza tangu wadogo na kufuata maelekezo ya wakufunzi wao.
Naye
Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi nchin Bw. Salum Chama akiongea na wandishi wa
habari kabla ya kumkaribisha katibu mkuu, amesema malengo yao ni kuhakikisha
Tanzania inakuwa na waamuzi wa kimataifa wengi.
Mwaka
huu Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kutoa waamuzi 18 wenye beji za FIFA
barani Afrika, nyuma ya Misri yenye waamuzi 22, Lengo ni kuhakikisha tunawaanda
vijana wengi waje kuwa waamuzi wa kimataifa.
Semina
hiyo ya siku 5 inatarajiwa kufungwa ijumaa tarehe 17 Mei, 2015
inajumuisha vijana kutoka mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Zanzibar, Mwanza,
Arusha na Mbeya, kati ya vijana 37 waamuzi wawili ni wanawake.
Wakufunzi
wa semina hiyo ni Soud Abdi, Riziki Majala na Joan Minja.
0 COMMENTS:
Post a Comment