KASEKE (WA KWANZA KULIA) AKIWA NA KIKOSI CHA MBEYA CITY. |
Kama kweli Simba na Yanga zinataka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Mbeya City, Deus
Kaseke basi zijiandae kuvunja benki na kumlipa daua la shilingi milioni 45 ili ajiunge
na moja kati ya timu hizo.
Mkataba
wa Kaseke na Mbeya City unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu, tayari Simba na
Yanga zimeshaonyesha nia ya kumsajili Kaseke lakini zilishindwa kuvunja mkataba
wake Desemba, mwaka jana katika dirisha dogo la usajili.
Kwa
mujibu wa kanuni, Kaseke anaruhusiwa kufanya mazungumzo na timu yoyote yenye
nia ya kumsajili na rafiki wa karibu wa winga huyo, aliliambia Championi
Jumamosi kuwa; “Kaseke anataka shilingi milioni 45 ili aweze kusaini Simba au
Yanga.
“Pia
anataka alipwe mshahara mzuri ambao watakubaliana na kulipiwa nyuma ya kuishi
jijini Dar, lakini bado anatoa nafasi kwa timu yake ya Mbeya City kama nayo
itakubaliana naye kuhusu usajili mpya.”
Alipotafutwa
na gazeti hili, Kaseke alithibitisha kuzungumza na Simba na Yanga na kuongeza; “Soka
ndiyo ajira yangu kama kuna timu itakuwa na mimi sina kinyongo lakini kwa sasa
natazama mechi yetu na Yanga ya
keshokutwa (kesho).”
0 COMMENTS:
Post a Comment