Baada ya kufikisha mabao 9, sasa Tambwe anataka kupambana na kutetea taji lake la mfungaji bora alilolipata msimu uliopita kwa kupachika mabao 19 wakati akiichezea Simba.
Mwenzake Simon Msuva wanayekipiga Yanga anaongoza kwa kuwa na mabao 13, lakini Tambwe raia wa Burundi amesisitiza akizubaa, basi ana "muovateki".
“Bado
sijakata tamaa na naamini nina kila sababu ya kutetea tuzo ya ufungaji bora,
ukiangalia hata pengo lililopo kati yangu na Msuva anayeongoza kwa kufunga siyo
kubwa, akijichanganya tu nitampita,” alisema Tambwe.
Hata
hivyo, Tambwe yupo nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji wa ligi hiyo kwani
nafasi ya pili wapo Didier Kavumbagu wa Azam FC na Rashid Mandawa wa Kagera
Sugar wenye mabao kumi kila mmoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment