Hali si nzuri kwa mbaya kwa Mtibwa Sugar na Prisons katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, lakini
timu hizo zimekomaa na kusema hazitakubali kushuka daraja.
Prisons
inashika mkia katika ligi hiyo yenye timu 14 ikiwa na pointi 20 na Mtibwa ipo
nafasi ya 12 ikiwa na pointi 23, zote zimecheza mechi 20 na zina michezo sita
tu.
Kocha
wa Mtibwa, Mecky Maxime alisema; “Nitapambana ili tusishuke daraja japokuwa
ligi ni ngumu na matokeo mengine yanakatisha tamaa kwani kila mara tunajipanga
kupata ushindi lakini mambo yanageuka.”
Kwa
upande wake, Ofisa Habari wa Prisons, Lupyuto Mwanguku alisema kikosi chao
kinapambana kupata pointi 18 katika mechi zake sita zilizobaki ili kisishuke
daraja.
“Kweli
ligi ngumu na tumebakisha mechi sita tu, tunataka tushinde zote ili kujiweka
katika nafasi nzuri ya kubaki katika ligi na hilo linawezekana,” alisema
Mwanguku.
Mtibwa,
leo Jumamosi inacheza na Azam FC kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, wakati Prisons
itacheza na Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
0 COMMENTS:
Post a Comment