April 9, 2015


Kikosi kizima cha Simba kitafanya ziara katika kituo cha kulelea watoto kisoka cha Marsh Academy jijini Mwanza.


Simba itatembelea katika kituo hicho kilichopo jijini Mwanza kwa lengo la kumuenzi marehemu Sylvester Marsh, mmoja wa waliokuwa makocha bora wazalendo.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema wanakwenda kwenye kituo hicho kuonyesha wanamuenzi Marsh lakini kuonyesha Simba inajali ukuzwaji wa wachezaji vijana.

"Kuhusiana na vijana, Simba ni timu inayojali vijana na ndiyo timu inaongoza kutumia vijana hata katika kikosi chake kikubwa.

"Hivyo tutafika pale kutembelea kituo hicho, tutatoa rambirambi na kumuenzi Marsh ambaye alitoa mchango mkubwa kwa vijana wakati wa uhai wake," alisema Manara.

Marsh alifariki wiki chache zilizopita jijini Dar es Salaam kutokana baada ya kusumbuliwa muda mrefu na ugonjwa wa kansa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic