Uongozi wa klabu ya Stand United, umeweka wazi kila kitu kuhusiana na uamuzi wake wa kutaka kumsajili kipa mkongwe Juma Kaseja.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Ufundi wa Stand, Muhibu Kanu amesema tayari wameanza mazungumzo na Kaseja kupitia meneja wake.
"Kweli tuna mpango huo, tunataka kikosi imara ambacho kitacheza michuano ya kimataifa msimu ujao.
"Kaseja ni kati ya wachezaji wanaoweza kutifikisha mbali lakini tunafanya juhudi ya kuhakikisha tunacheza ligi kuu tena msimu ijao.
"Baada ya hapo tutaendelea na mazungumzo na Kaseja. Atakachohitaji tutajitahidi kumpa ili aweze kutusaidia," alisema Muhibu.
Stand ni kati ya timu zinazopambana kuhakikisha zinabaki Ligi Kuu Bara.
Iko katika nafasi ya 11 ikiwa na pointi 24 hivyo inahitaji kushinda angalau mechi tatu kujiweka pazuri na uhakika wa kubaki.
0 COMMENTS:
Post a Comment