Kocha Mkuu wa Yanga,
Hans van der Pluijm amejigamba kuwa kikosi chake ni kipana na kinaweza
kupambana na mazingora tofauti.
Pluijm raia wa
Uholanzi amesema kikosi chake kiko katika hali nzuri kwa kuwa wachezaji wengi
wako fiti.
“Kuumia kwa
wachezaji kunatokea hasa kutokana na ugumu wa mechi mnazokuwa mnacheza. Hilo
halikwepeki hata kidogo.
“Lakini kama angalau
utakuwa na uhakika wa kuchagua wachezaji wawili au watatu katika kila nafasi.
“Pamoja na hivyo,
inakuwa bora zaidi kama wachezaji wote wanakuwa fiti. Unakuwa na uhakika ucheze
aina fulani ya mfumo kulingana na unavyotaka.
“Kinachonifurahisha
kwa sasa ni namna wachezaji wanavyopambana, wanajua tunataka nini na nini
kifanyike sasa,” alisema Pluijm akionekana kuwa na uhakika.
Yanga inaongoza Ligi
Kuu Bara ikiwa na pointi 43, inafuatiwa na Azam FC 38 na Simba nafasi ya tatu
ikiwa na 35.
0 COMMENTS:
Post a Comment