Na
Saleh Ally
SWALI
la kwanza, unawazuia vipi Juventus wasiwe mabingwa wa Italia, maarufu kama
Serie A?
Hadi
sasa wana pointi 70 wakiwa ndiyo vinara wa msimamo wa Serie A. Wanaowafuatia AS
Roma wana pointi 56, tofauti ya pointi 14.
Mechi
zilizobaki ni tisa tu, Juventus itacheza nne nyumbani na tano ugenini huku
mfumo ukionyesha itakuwa hivi, mechi moja nyumbani, moja ugenini hadi
watakapomaliza.
Kama
Roma watashinda mechi zao zote tisa zilizobaki watafikisha pointi 83. Maana
yake Juve wanatakiwa kushinda mechi tano kati ya tisa wajihakikishie ubingwa
maana watakuwa na pointi 85.
Uwezo
wa kushinda mechi hizo wanao? Takwimu za mechi sita zilizopita zinawabeba kwa
kuwa wameshinda mechi tano na kutoka sare moja.
Timu
inayoonekana kuwa na rekodi nzuri zaidi ya Juve kwa mechi sita zilizopita ni
Lazio ambayo imeshinda zote, hata hivyo iko katika nafasi ya tatu ikiwa na
pointi 55, bado haiwezi kuwa presha kwa Juve.
Takwimu
za mechi hizo zilizopita zinaonyesha kuwa Juve tayari imeusogelea kwa mara
nyingine ubingwa wa Italia kwa asilimia 90.
Ubora
wa kikosi chake unaoongozwa na Carlos Teves ambaye ameshaifungia timu hiyo
mabao 17, unaonyesha hawatazuilika na wenyewe ndiyo wamiliki wa Italia katika
soka.
Ufalme
wa Juve unaonekana kuzidi kutanuka na kuimarika zaidi kutokana na wakongwe
wengine kupoteza kabisa mwelekeo.
Wakongwe
wenzake, yaani AC Milan na Inter Milan ni choka mbaya kabisa, maana wapo katika
nafasi ya za nane na tisa katika msimamo huo wa timu 20.
Hadi
sasa Juve ndiyo timu yenye safu kiwembe ya ushambuliaji, imefunga mabao 57 na
ina ngome ngumu, imefungwa 14 tu huku iliyofungwa mengi zaidi ikiwa ni Cagliari
iliyotunguliwa mara 56.
Juve
imefunga mabao 36 na 26 yakiwa ni ya ugenini. Imefungwa saba ugenini na saba
nyumbani kukamilisha hiyo 14 ambayo ni idadi ndogo zaidi msimu huu.
Kiungo
kinachoongozwa na mkongwe Andrea Pirlo na bwa’mdogo Paul Pogba, kinaifanya Juve
kuwa timu iliyounganika vema.
Kwa
hali inavyokwenda, inaonekana hakuna wa kuizuia Juve kutwaa ubingwa wa 31 wa Serie
A. Soka ni mchezo wenye maajabu yake, lakini nafasi ya Juve ni kubwa zaidi
huenda zaidi hata ya maajabu ya soka.
MISIMAMO
LIGI:
1
Juventus 29 70
2 AS Roma 29 56
3
Lazio
29 55
4 Fiorentina 29 49
5
Sampdoria 29 48
NYUMBANI:
1
Juventus 15 41
2
Lazio 14 30
3 AS
Roma
15
30
4
Sampdoria 14 28
5
Napoli
14
26
UGENINI:
1
Juventus 14 29
2 AS
Roma 14
26
3
Lazio 15 25
4
Fiorentina 15 25
5
Torino 15 21
MECHI SITA ZA MWISHO:
Februari 20:
Juventus 2-1
Atalanta
Machi
2:
AS
Roma
1-1
Juventus
Machi
9:
Juventus 1-0
Sassuolo
Machi
14:
Palermo 0-1
Juventus
Machi
22:
Juventus 1-0
Genoa
Aprili
2:
Juventus 2-0 Empoli
TAKWIMU:
NYUMBANI
UGENINI
Ushindi 13….87%
8….
57%
Sare 2 ….13%
5….
36%
Poteza 0 …. 0%
1….
7%
JUMLA 15 14
Fin.
0 COMMENTS:
Post a Comment