Nyota
wa zamani wa soka wa klabu ya Barcelona ya Hispania, leo Jumamosi wanacheza
mechi ya kirafiki na wanasoka wa zamani wa Tanzania kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Baadhi
ya nyota hao; Patrick Kluivert, Gaizka Mendieta , Anderson De Soursa ‘Deco’,
Francesco Coco na Luis Garcia, waliwasili jana Ijumaa jijini Dar es Salaam kutoka
Zanzibar.
Baadhi
ya wachezaji hao jana walikuwa Zanzibar kwa mwaliko maalum wa Rais wa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein. Hao ni Simao Sambrosa, Mendieta,
Garcia, Luis Enrique, Kluivert na Johan Cruyff.
Kocha
wa timu hiyo, Cruyff alisema kuwa wamekuja kuonyesha vipaji vyao vya zamani na
hakuna wa kuwazuia kushinda katika mechi ya leo.
“Tupo
vizuri, tumejiandaa kwa ajili ya kuweka historia, tunajua wenyeji wataleta
upinzani, lakini sisi ndiyo tutakuwa washindi,” alisema Cruyff.
Mratibu
wa mechi hiyo kutoka Kampuni ya Primetime Promotions, Stuart Kambona, alisema
maandalizi yamekamilika na kikosi cha Tanzania kitakuwa na nyota wa zamani kama
Peter Manyika, Juma Kaseja, Shadrack Nsajigwa, Abubakari Kombo, Mustapha Hozza,
Salvatory Edward, Dua Said na Yusuph Macho.
Wengine
kwa mujibu wa Kambona ni Shaban Ramadhan, Dua Saidi, Nassoro Bwanga, Mohamed
Hussein, Steven Nyenge, Mwanamtwa Kihwelu, Edibily Lunyamila, Henry Morris,
Haruna Moshi, Bitta John, Madaraka Selemani, Deo Lucas, Bakari Malima, Thomas
Kipese, Khatibu Sinapo na Nico Nyagawa.
Kambona
alitaja viingilio katika mchezo huo kuwa ni Sh 7,000 kwa viti vya kijani,
Sh10,000 (Bluu), Sh 20,000 (Machungwa), Sh30,000 (VIP C), Sh 50,000 (VIP B) na
Sh 300,000 kwa VIP A.
0 COMMENTS:
Post a Comment