JULIO |
Yule Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Yanga, Jerry Muro, kweli haishiwi maneno!
Safari hii ameibuka na mpya akimtaka Kocha wa muda wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo 'Julio' kuacha kurukia mambo na sasa arejee kuifundisha timu ya Mwadui FC aliyoipandisha daraja.
MURO |
Akizungumza na SALEHJEMBE, Muro amesema Julio alipaswa kutulia baada ya kuipandisha Mwadui FC na si kuirukia Coastal Union kama alivyofanya.
"Sijui ndugu yetu Julio aliendea nini Coastal Union, sasa ona kilichomkuta. Aibu kwake, ndiyo maana nashauri asiwe anarukia tu mambo," alisema Muro akionyesha kujiamini baada ya Yanga kuikung'uta Coastal Union kwa mabao 8-0, jana.
Baada ya kuipandisha Mwadui FC kucheza Ligi Kuu Bara, Julio aliingia katika benchi la ufundi kwa lengo la kuinusuru Coastal Union.
Hali hiyo ilisababisha kocha Mkenya, James Nandwa kuachia ngazi na Julio akakabidhiwa jukumu kamili.
Lakini jana, mambo yalikuwa mabaya baada ya kutandikwa mabao hayo nane kwa mtungi.
Na bado watafungwa sana tu maana wamepoteza mwelekeo kabisa.
ReplyDelete