Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amesema anaamini alipaswa
kupewa shukurani kutokana na kuwa wa kwanza kusisitiza klabu yake inapaswa
kumuacha straika Amissi Tambwe.
Tambwe alijiunga
na Yanga, siku moja tu baada ya kuachwa na Simba na amekuwa akionyesha mwelekeo
mzuri.
Katika mahojiano
maalum Hans Poppe, alisema Tambwe amekuwa na bahati na Yanga na mambo
yanakwenda vizuri kwa kuwa aliachwa na Simba.
“Angebaki Simba,
huenda bado angekuwa hafanyi vizuri. Lakini sioni kama kuna sababu ya kuendelea
kulaumu kuhusiana na sisi kumuacha, badala yake watushukuru, tumemuacha na
kaenda Yanga, sasa mambo mazuri,” alisema Hans Poppe.
“Nafikiri leo ni wakati mwafaka wa kuweka hili wazi, kwamba mimi ndiye
niliyesisitiza Tambwe aondolewe. Kweli Phiri hakutamka tumuondoe, lakini
alisema vitu vinavyomaanisha kwamba hamhitaji.
“Mazungumzo ya Phiri yalionyesha wazi hakuwa anamhitaji Tambwe. Phiri
aliniambia kwa mfumo wake mchezaji wa box (anayesubiri kufunga) hawezi kufanya
vizuri.
“Sasa kulikuwa na haja gani ya kuendelea kubaki naye akiwa hachezi? Leo
yupo Yanga anacheza,” alisisitiza Hans Poppe.
Tambwe alikuwa mfungaji bora msimu uliopita kwa kufunga mabao 19 akiwa
na Simba ambayo alijiunga nayo akitokea Vital’O ya Burundi.
0 COMMENTS:
Post a Comment