Yule mshambuliaji
aliyekuwa anatakiwa kwa udi na uvumba na Simba, imeelezwa ameishakubaliana na
Azam FC ambao walikuwa wakimuwania kwa juhudi zote.
Straika huyo, Mohammed
Traore wa El Merreikh ya Sudan amekuwa akifanya mazungumzo na Azam FC kwa
kipindi kirefu. Lakini Simba nayo ilikuwa ikijipenyeza kuonyesha inamhitaji.
Simba sasa inataka
kusajili straika mwenye uwezo mkubwa wa kuzifumania nyavu na Traore raia wa
Mali ndiye aliyeonekana anafaa lakini Azam imewawahi kwa kumsajili ili kujiweka
vizuri.
Taarifa zinasema straika
huyo mwenye umri wa miaka 26, tayari amekubali kutua Azam FC baada ya wenyewe
kuonyesha wako ‘siriaz’.
Aliwahi kuzichezea klabu
kubwa kama Ismaily ya Misri na baadaye Al-Hilal ya Sudan kabla ya kutua El
Mereikh msimu wa 2013/2014.
Simba ilifanya mazungumzo
na Traore, kwa mara ya kwanza alipokuja nchini kucheza dhidi ya Azam katika
Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Azam Complex. Mkataba wa Traore na El
Merreikh unaisha mwezi ujao.
Mmoja wa mabosi wa Simba
katika kamati ya usajili alisema; “Tulikuwa tumeshamaliza kila kitu na Traore
na tulitegemea tungekuwa naye msimu ujao ili kuimarisha kikosi chetu.”
Rafiki wa karibu wa
Traore kutoka Sudan, amelithibitishia Traore kusaini Azam kwa kusema; “Traore
amesaini Azam na hana mpango wa kubaki El Merreikh.”
0 COMMENTS:
Post a Comment