Rais wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameitakia kila la kheri
timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania (Twiga Stars) katika mchezo wake wa kesho wa
marudaino dhidi ya timu ya Taifa ya Zambia (She-Polopolo) utakaochezwa Uwanja
wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akizungumza na
wachezaji wa Twiga Star na benchi la Ufundi katika chakula cha pamoja cha
mchana leo katika hosteli za TFF zilizopo Karume, Rais Malinzi amesema
watanzania wote wana matumaini na timu yao kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa
marudiano.
Aidha Rais
Malinzi amewaambia bechi la ufundi na wachezaji wa Twiga Stars kuwa pesa zote
zitakazopatikana katika mchezo wa kesho baada ya makato ya Uwanja na VAT,
wagawane kwa pamoja wachezaji na viongozi.
Naye Mgeni
mualikwa Ryhs Torrington ambaye ni Mkurugenzi wa kituo cha Luninga cha Azam,
alisema anaitakia kila la kheri Twiga Stars katika mchezo wao wa kesho, na
kusema mechi hiyo itaonyeshwa moja kwa moja na Azamtv, hivyo waitumie vizuri
nafasi hiyo kujitangaza kimataifa.
Kocha mkuu
wa Twiga Stars Rogasian Kaijage na nahodha wake Sophia Mwasikili,
wamewahakikishia ushindi katika mchezo wa kesho, na kuwaomba watanzania
kujitokeza kwa wingi uwanjani kuja kuwashangilia.
Mechi
inatarajiwa kuanza majira ya saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki, na
tiketi za mchezo zitauzwa kesho saa 2 asubuhi eneo la Uwanja wa Taifa jijini
Dar es salaam, huku viingilio vya mchezo huo vikiwa ni tsh. 5000 kwa VIP na
tsh. 2000 kwa majukwaa yaliyobakia.
Twiga Stars
ambayo katika mchezo wa awali iliibuka na ushindi wa mabao 4-2, inahitaji sare
ya aina yoyote ili kuweza kufuzu kwa fainali za Michezo ya Afrika
zitakazofanyika nchini Congo-Brazzavile mwezi Septemba.
0 COMMENTS:
Post a Comment