Mbunge wa Mbeya Mjini,
Joseph Mbilinyi amewataka mashabiki wa Mbeya City kutokata tamaa kutokana na
mwenendo wa timu yao msimu huu.
Mbilinyi maarufu kama Sugu
amesema upepo mbaya umepita Mbeya City msimu huu na ana imani kikosi kitafanya
vema zaidi.
“Mimi ndiyo mbunge wao,
Mbeya City, najua watu wana mapenzi makubwa na timu yao. Viongozi nao
wanapambana.
“Mimi ni shabiki mkubwa,
ndiyo maana nina imani mambo yatakwenda vizuri msimu ujao.
“Wana Mbeya wanapaswa
kusaidiana pia kuwa wavumilivu katika kipindi hiki,” alisema.
Pia Sugu alitoa shukurani
kwa wadhamini wao Bin Slum Tyres Ltd kutokana na udhamini wao.
“Ni watu wanaotakiwa kupewa
shukurani, wameiamini Mbeya na Wanambeya wanaijua dhamani yao.
“Tunaamini tutaendelea kuwa
nao, lengo ni kuisaidia timu hiyo ya Wanambeya,” alisema.
Kampuni ya Bin Slum ndiyo wadhamini wakuu wa Mbeya City kupitia betri zao za RB.
Mbeya City ilifanya vema
msimu uliopita, lakini ikashindwa kurejea msimu na mwendo wake kuwa wa
kusuasua.
0 COMMENTS:
Post a Comment