Kocha Hans vand der Pluijm
amesema watapambana bila ya kuwa na wachezaji wao kadhaa ambao wana matatizo
mbalimbali.
Yanga imeondoka jana usiku
kwenda Tunisia kupitia Dubai kwenda kuwavaa Etoile du Sahel katika mechi ya
pili ya Kombe la Shirikisho.
Pluijm amesema wako katika
hali nzuri lakini kuna ugumu wa kuwakosa baadhi ya wachezaji.
Baadhi ya walioachwa ni
pamoja na Hassan Dilunga, Salum Telela na Danny Mrwanda.
“Kweli wengine wanabaki
wakiwemo wachezaji muhimu. Lakini hakuna kinachoshindikana, kikubwa ni
kupambana.
“Wote tunajua ni mechi
ngumu. Lakini ni lazima tucheze kwa umakini mkubwa, tunaweza kupambana,”
alisema Pluijm, dakika chache kabla ya kuondoka.
GOD BLESS YOU.
ReplyDelete