Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), limeiamuru klabu ya Ndanda SC kumlipa mchezaji Amiri S. Msumi
kiasi cha Sh 2,600,000.
Pia Kamati ilihoji
mkataba kutokuwa na kipengele cha mshahara, na kusema ni lazima mkataba
uonyeshe Kaiser ambacho mwajiriwa analipwa.
Pia Kamati ya Sheria na
Hadhi za Wachezaji za shirikisho imeagiza kuwa klabu zifahamishwe kuwa fedha ya
kusaini mkataba (sign on fee) hazitakiwi kulipwa kwa mafungu.
Tafsiri ya fedha ya
kusaini, ni mchezaji kulipwa fedha yote baada ya kusaini, na si kwa mafungu.
Pamoja na uamuzi huo, Katibu Mkuu wa Ndanda SC ametakiwa kuwepo kwenye kikao
cha Mei 3, 2015.
Malalamiko mengine
yataendelea kusikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Mei 3, mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment