Na
Saleh Ally
UKIMSIKILIZA
Masau Bwire wakati amewageuzia Yanga kibao na kuanza kuwapa hadithi ya mvuvi na
nyavu zake, utasikia raha na kuona kuwa soka, lina raha hata nje ya uwanja.
Msemaji
huyo wa Ruvu Shooting alitamba kwamba wangeisimamisha Yanga katika mechi yao ya
Ijumaa iliyopita, lakini kikosi chake kikaambulia kipigo cha mabao 5-0 huku
yeye akiwa jukwaani hoi.
Masau
ni shujaa, ana uwezo wa kuzungumza na kuipoteza historia inayojengwa na rekodi
kwamba Ruvu Shooting ndiyo wateja wakubwa wa Yanga katika kipindi cha misimu
minne iliyopita ya Ligi Kuu Bara.
Timu
hizo zimekutana mara nane tu katika misimu hiyo minne katika mechi za Ligi Kuu
Bara lakini ndiyo timu ambayo Yanga imeitungua mabao mengi kuliko nyingine.
Takwimu
zinaonyesha kuanzia msimu wa 2011-12 hadi 2014-15, Yanga imekutana na Ruvu
Shooting na kuifunga mabao 19 huku Wanajeshi hao wakiwa wamezitikiza nyavu za
Yanga mara tatu tu.
Huenda
Ruvu Shooting ndiyo wanyonge wa Yanga kuliko timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu
Bara kwa misimu yote hiyo minne.
Msimu
wa 2011-12, Yanga iliifunga Shooting jumla ya mabao 2-1 katika mechi zote
mbili. Msimu uliofuata katika mechi mbili Yanga ikapata mabao 4-2 dhidi ya timu
hiyo ya jeshi.
Katika
misimu miwili ya mwisho, inaonekana mambo yalizidi kuwa mabaya zaidi kwa kikosi
cha Masau Bwire kwa kuwa wateja wa Yanga rasmi huku wakichapwa rundo la mabao.
Msimu
wa 2013-14, katika mechi zote mbili, Yanga ikapata jumla ya mabao 8-0 dhidi ya
Shooting na msimu huu, Yanga inayoelekea kutwaa ubingwa ikapata jumla ya mabao
5-0 dhidi ya Shooting ambayo katika mechi ya kwanza ya msimu ilijitutumua kwa
matokeo ya 0-0 halafu ikaachia mzunguko wa pili, ikalambwa tano bila majibu.
Kinachovutia
zaidi, katika mabao 19 ambayo Yanga imeifunga Shooting katika misimu hiyo mine,
wageni ndiyo wameonekana “wanazifahamu” zaidi nyavu za timu hiyo ya jeshi,
kwani wamefunga mabao 13 huku wenyeji wakifunga 6 tu.
Waliofunga
mabao hayo ni kuanzia Kenneth Asamoah (Ghana), Davies Mwape (Zambia), Hamis
Kiiza & Emmanuel Okwi (Uganda), Mbuyu Twite (Rwanda), Didier Kavumbagu
& Amissi Tambwe (Burundi) na Kpah Sherman (Liberia).
Wageni
hao kutoka nchi sita wakiongozwa na Kavumbagu aliyefunga mabao matatu ambayo ni
mengi zaidi, ndiyo wameisambaratisha kabisa Ruvu Shooting.
Wenyeji
wanaongozwa na Simon Msuva aliyefunga jumla ya mabao manne katika misimu hiyo
na mengine mawili yamefungwa na Mrisho Ngassa na Jerry Tegete, hivyo
kukamilisha mabao sita ya wazalendo.
Masau
ni jasiri kwa kuwa anaweza “kuichanyata” rekodi hiyo hadi kuifanya Ruvu
Shooting kuwa mpinzani mkubwa wa Yanga.
Inawezekana
hakuzisoma, lakini akitulia atagundua lazima wabadili gia na kuweka kubwa
kwelikweli ili kujiondoa kwenye jina la “wateja maarufu wa Yanga”.
JUMLA
YA MABAO KWA MISIMU:
2011-12:
Yanga
2-1 Ruvu
2012-13:
Yanga
4-2 Ruvu
2013-14:
Yanga
8-0
2014-15:
Yanga
5-0
WALIOIFUNGA ZAIDI:
WAGENI (bao 13):
Kavumbagu
3
Kiiza
3
Sherman
2
Asamoah
1
Mwape 1
Twite
1
Okwi
1
Tambwe
1
WENYEJI (bao 6):
Msuva
4
Tegete
1
Ngassa
1
2011-12
Septemba
10, 2011
Yanga
1–1 Ruvu
Asamoah
Dk 75 Paul Ndauka Dk 69
Februari
12, 2012
Ruvu 0-1 Yanga
Davies Mwape Dk 47
2012-13
Oktoba
20, 2010:
Yanga
3-2
Ruvu
Chamazi
Twite Dk
20
Seif Abdallah Dk 2
Tegete
Seif Abdallah Dk 9
Kavumbagu
64
Machi
16, 2013:
Ruvu
0-1
Yanga
Taifa
Hamis Kiiza Dk 48
2013-14
Septemba
28, 2013:
Yanga 1-0
Ruvu
Taifa
Kiiza
Dk 63
Februari
22, 2014:
Ruvu
0-7
Yanga
Taifa
Kavumbagu Dk 1
Msuva Dk 2
Okwi 28
Ngassa 34
Kavumbagu Dk 53
Kiiza Dk 64
Msuva 77
2014-15
Januari
17, 2015:
Yanga
0-0
Ruvu
Taifa
Aprili
24, 2015:
Ruvu
0-5
Yanga
Taifa
Msuva Dk 15
Sherman Dk 24
Msuva Dk 45
Tambwe Dk
57
Sherman Dk 67
0 COMMENTS:
Post a Comment