Mambo yameanza Tanga
kwani African Sports imeiingilia Mgambo JKT na inataka kumchukua kocha wake
Bakari Shime ili awafundishe msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
African Sports ambayo ni
hasimu mkubwa wa Coastal Union, imefanikiwa kupanda ligi kuu ikitokea Ligi Daraja
la Kwanza na mpango wao wa kwanza ni kuhakikisha wanakuwa na Shime msimu ujao.
Meneja wa African Sports,
Ahmed Boznia: “Tunataka kumchukua Shime ili tuwe na kikosi imara, tayari
tumeshafanya mazungumzo naye na muda wowote tutafikia muafaka.”
Alisema wameongea na
kocha huyo lakini amewataka wamsubiri apumzike kidogo baada ya kumaliza ligi
ndipo baadaye waendelee na mazungumzo hayo.
Alipotafutwa Shime
alisema: “Siwezi kusema lolote kuhusu jambo hilo, naomba umtafute meneja wangu
Binslum (Nassor) atakuambia kila kitu.”
Binslum alipotafutwa
alisema hayupo katika nafasi ya kuzungumzia jambo hilo kwa sasa.
Simba yapigwa chini
Kagame Cup
0 COMMENTS:
Post a Comment