Kesho Jumapili uongozi wa
Ndanda FC ya Mtwara utakutana kujadili taarifa ya kocha wao, Meja Mstaafu,
Abdul Mingange juu ya ushiriki wao wa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara pia kujua
matakwa ya kocha msimu ujao.
Ndanda imenusurika
kushuka daraja msimu huu, baada ya kukutana na ushindani wa hali ya juu katika
ligi hiyo, hivyo inataka kufanya vizuri msimu ujao.
Katibu Mkuu wa Ndanda,
Selemani Kachele, ameliambia Championi Jumamosi: “Tumeshapata taarifa ya kocha
na Jumapili (kesho) tutaifanyia kazi ili kujua tutasajili kina nani na
tutawaacha kina nani.
“Hatutaki kuwa na kikosi
cha mashaka kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo ilibaki kidogo tushuke
daraja, hivyo tutakuwa makini na usajili.”
0 COMMENTS:
Post a Comment