Uongozi wa Stand United ya Shinyanga umefunguka
kuwa unamnyemelea beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde ambaye anadaiwa
kufuatiliwa na timu za Simba na Yanga.
Stand ambayo imepanga kujiimarisha zaidi katika
ligi msimu ujao baada ya kunusurika kushuka daraja, imeeleza kuwa inahitaji
kufanya usajili makini ili kuweza kuleta ushindani msimu ujao.
Muhibu Kanu ambaye ni Mkurugenzi wa Benchi la
Ufundi la Stand, amesema moja ya mikakati waliyojiwekea katika timu hiyo ni
kuhakikisha wanakuwa na kikosi kilicho bora zaidi, ndiyo maana wanaendelea
kusaka wachezaji wenye viwango vya juu.
“Tupo katika mazungumzo na Salum Mbonde ili
tumsajili, tunajua kwa sasa yupo katika timu ya taifa lakini atakaporejea nchini
ndiyo tutajua hatma yake.
“Tuna mikakati mikubwa kwa ajili ya msimu ujao,
kwani tunahitaji kuwa na kikosi bora kwa kusaka kipa imara ambapo kwa sasa
tunafanya mazungumzo na Juma Kaseja ili aweze kuziba pengo la kipa kutokana na
mtazamo wetu kuwa atatufaa, kwani malengo yetu ni kumaliza katika ‘top four’
msimu ujao.
“Kaseja mwenyewe ameonyesha nia ya kuja kuichezea
timu yetu ambapo ametutaka tufanye mazungumzo na meneja wake,” alisema Kanu.
0 COMMENTS:
Post a Comment