Kocha Goran Kopunovic amesema ataendelea kuwa
shabiki wa Simba kokote atakapokwenda.
Kopunovic raia wa Serbia amezungumza na
SALEHJEMBE kutoka jijini Budapest, Hungary na kusisitiza kuwa hakupenda
kuondoka Simba.
“Kweli sikupenda, lakini siwezi kulazimisha. Hivyo
waambie mashabiki wa Simba nitaendelea kuwapenda sana.
“Simba ilishaingia moyoni mwangu, lakini maisha
ya soka yako hivi mara zote,” alisema.
Simba imeamua kusaka kocha mwingine na sasa
imetoa nafasi kwa Mbelgiji baada ya kuonekana Kopunovic anataka dau kubwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment