Kocha wa zamani wa Simba, Patrick Liewig
amesema yuko tayari kurejea nchini na kuinoa Simba.
Liewig amesema anajisikia faraja kama atapata
nafasi hiyo ili atimize ndoto yake. Pia yuko tayari wakati wowote kwa ajili yao.
“Wakati ule niliondoka nikiwa ndiyo nimeanza
kufanya kile nilichokuwa nimekitaka.
“Kikosi changu hakikuwa kimefanya kazi vizuri
mwanzoni. Baada ya kambi ya Oman kulikuwa na mabadiliko kadhaa. Nikaona ndiyo
timu inaanza kuonyesha njia, nikaondolewa.
“Nikipata nafasi hiyo kwa sasa nina imani
nitafanya vitu vizuri kwa kuwa Simba ina watu wengi wanajua mpira,” alisema
Liewig.
Mfaransa huyo aliingoza Simba kwa nusu msimu,
tena ikiwa na kikosi chenye vijana wengi sana.
Simba iko katika harakati za kusaka kocha mpya
baada ya Goran Kopunovic “kuzingua” kwa kudai dau kubwa ambalo Simba wameona
hawaliwezi.
0 COMMENTS:
Post a Comment