Wakati Yanga ikipiga
hesabu za kusajili baadhi ya wachezaji kutoka timu za Ligi Kuu Bara kuimarisha
kikosi chake, winga wa zamani wa timu hiyo, Edibily Lunyamila amesema haina
haja kwa klabu hiyo kusajili wachezaji wa ndani.
Badala yake Lunyamila
akasisitiza, Yanga inapaswa kusajili wachezaji au mchezaji wa kigeni mzoefu ili
ifanye vizuri katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
“Najua Yanga itakuwa
inataka kujaza wachezaji wa kigeni ili kupunguza waliopo pia kuongeza nyota
wengine wa ligi ya nchini ili kukiongezea nguvu kikosi.
“Kuhusu hao wa kimataifa
sawa hakuna tatizo lakini ukiniambia kuhusu hapa nchini wala siafiki na sijaona
sababu ya Yanga kusajili mchezaji wa hapa nchini kwani wana kikosi kinachofanya
vizuri. Isajili mchezaji mgeni atakayecheza nafasi ya Ngassa,” alisema Lunyamila.
Wageni walio katika
hatari ya kusitishiwa mikataba yao ni Andrey Coutinho raia wa Brazil na Kpah
Sherman wa Liberia ambaye ameripotiwa kuhitajika na timu kadhaa nje ya nchi.
0 COMMENTS:
Post a Comment