| SHERMAN. |
Straika wa Yanga, Kpah
Sherman, ameweka unafiki pembeni na kusema nyota wa Simba, Emmanuel Okwi, kwa
jinsi anavyocheza uwanjani, ana uhakika wa kucheza soka popote pale hata nje ya
Afrika.
Sherman, raia wa Liberia
ambaye alitua Yanga Desemba mwaka jana akitokea Klabu ya Cetinkaya ya Cyprus,
amewahi kucheza timu moja na kiungo wa Mtibwa Sugar, Henry Joseph katika kikosi
cha Kongsvinger ya Norway.
Sherman amesema Okwi anajua majukumu yake uwanjani na kwa uwezo wake,
anaweza kucheza soka la kulipwa popote pale Afrika hata nje ya bara hili.
“Okwi ni rafiki yangu wa
karibu, anacheza kwa kujituma sana, anamiliki mpira, anatumia akili nyingi sana
uwanjani na vitu vingine vingi, ambavyo naweza kusema anaweza kucheza popote,”
alisema Sherman ambaye ameifungia Yanga mabao sita tangu alipojiunga nayo.
Wakati huohuo, Sherman
alisema pengo la winga Mrisho Ngassa aliyejiunga na Free State kwa dau la dola
150,000 (Sh milioni 300) katika timu yao, linahitaji mtu makini kuliziba,
vinginevyo timu haitakuwa imara.







0 COMMENTS:
Post a Comment