May 22, 2015



Uongozi wa Klabu ya Simba umemtega kiungo wake mshambuliaji, Ramadhan Singano ‘Messi’ kwa kumtaka atafakari kwa mara nyingine kuhusu dau la shilingi milioni 30 alilotajiwa, badala ya shilingi milioni 50 anazotaka.

Singano ambaye alipandishwa kutoka kikosi cha Simba B, inaelezwa kuwa anatembea na mkataba aliopewa kwa kuwa anahitaji kutafakari kabla ya kusaini.

"Tumempa mkataba, alisema anataka kuwapa watu wake wa karibu wauangalie na kumshauri, hivyo tumempa afanye hivyo," alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe.

Hata hivyo kumekuwa na taarifa kwamba uongozi wa Simba umekuwa katika mikakati ya kuachana na wachezaji wote wanaousumbua.

Hivyo kama Messi ataendelea kuusumbua kwa madai ya kuongezewa dau kubwa zaidi kwa kuwa tu Jonas Mkude alilipwa dau kubwa, basi utaachana naye na kuangalia njia nyingine.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic