Hali inaonekana kuwa si shwari katika kikosi cha
timu ya taifa, Taifa Stars, ambapo inadaiwa kuwa kuna mgawanyiko ndani ya
kikosi hicho ambacho kipo katika michuano ya Cocafa nchini Afrika Kusini.
Baadhi ya wachezaji wa Stars wamezungumza na SALEHJEMBE na kusema hawafurahishwi na jinsi timu hiyo inavyocheza na kudai
kuwa kila wanapomshauri kocha wao, Martin Nooij amekuwa haelewi somo, ndiyo
maana wanafanya anavyotaka yeye.
“Tumemwambia mara nyingi kuwa sisi wachezaji
tunajuana wenyewe lakini amekuwa mbishi,” alisema mchezaji mmoja.
Upande wa Nooij akizungumzia matokeo mabaya ya
Stars katika Cosafa, alisema mashindano hayo hayakuwa na umuhimu kwake na
badala yake anatumia kama maandalizi ya kucheza na Misri.
Wakati huohuo, Stars inatarajiwa kurejea nchini
leo usiku mara baada ya mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya Lesotho
utakochezwa leo jioni.
Aidha, Kamati ya Utendaji ya TFF inatarajiwa
kukutana keshokutwa Jumapili ambapo moja ya ajenda itakua ni kupokea na kujadili
mienendo, maandalizi na maendeleo ya timu za taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment