ABOAGYE (MWENYE JEZI YA NJANO, NAMBA 4) AKIWA NA MSHAMBULIAJI WA YANGA, SHERMAN, WAKALA WAKE NA MCHEZAJI MWINGINE AMBAYE AMELETWA KUFANYA MAJARIBIO YANGA. |
Mwezi uliopita, Simba ilimshusha straika anayetajwa kuwa hatari katika kufumania
nyavu, Mghana, Aboagye Gerson, hata hivyo baada ya ligi kumalizika, ilidaiwa
kuwa amerejea kwao, lakini imegundulika kuwa nyota huyo bado yuko Dar, lakini
anashinda, analala na kufanya mazoezi na wachezaji wa Yanga.
Nyota
huyo yupo Dar akiendelea kujifua kwenye uwanja uliopo maeneo jirani na Kituo
cha Daladala cha Simu2000, kwa ajili ya kujiweka fiti.
Simba
ndiyo inamgharimia kila kitu kwa kumtunza, ambapo inasemekana analala kwenye
hoteli moja iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam.
Chanzo
cha kuaminika kimesema kuwa kwa muda mrefu nyota
huyo amekuwa akipasha uwanjani hapo pamoja na wachezaji wengine wa Yanga,
akiwemo Kpah Sherman na nyota wa Sierra Leone, Lansana Kamara, ambaye inaelezwa
ameletwa kufanya majaribio Yanga.
Nyota
huyo alitua Msimbazi akitokea Klabu ya Zhakoya ya nchini Iraq, alifanya mazoezi
na Simba mwishoni mwa ligi msimu uliomalizika chini ya Mserbia, Goran
Kopunovic.
“Mbona
yupo hapa Bongo na anafanya mazoezi na kina Sherman pale uwanja uliopo karibu
na Kituo cha Simu2000 na amepangishiwa pale (anaitaja hoteli), kila wakati
utamuona na wachezaji hao wa Yanga.
“Inaelezwa
kuwa yeye na huyo jamaa wa Sierra Leone wanalala hoteli moja na wakati wote
wamekuwa pamoja,” alisema mtoa habari wetu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, alipotafutwa kutolea
ufafanuzi suala hilo, alisema yuko bize na ametingwa na kazi nyingi kisha
akakata simu, wakati rais Evans Aveva, simu yake haikupokelewa licha ya
kupigiwa mara kadhaa.
0 COMMENTS:
Post a Comment