Uongozi
wa Mtibwa Sugar umesema haupo tayari kumuuza kipa wake Said Mohammed kwenye
kikosi cha Azam FC.
Hivi
karibuni iliripotiwa kuwa kipa huyo anaweza kwenda Azam kwa mshahara wa Sh
milioni mbili kwa mwezi na dau la usajili milioni 30.
Kipa
huyo amekuwa akihusishwa kuwa huenda akatua katika Klabu ya Azam FC na
ikishindikana timu yake ya zamani ya Yanga.
Ofisa habari wa timu hiyo, Thobias Kifaru, alisema kuwa
kipa huyo ni mali yao na haendi popote, ataendelea kuitumikia timu hiyo huku
wakimkaribisha nyumbani aliyekuwa kipa wa timu hiyo, Hussein Sharifu ‘Cassilas’.
“Said
Mohamed atabaki kuwa mali yetu na haendi popote, kwa sasa tumembadilisha kwa
kiasi kikubwa na wengine sasa ndiyo wameanza kumtolea macho, ataendelea
kuitumikia timu yake kama kawaida, hayo yanayoendelea sasa ni maneno tu.
“Na
tumekuwa na kawaida ya kutengeneza makipa bora kutokana na uwezo wa kocha wetu
ambaye hata timu ya taifa imemuamini na kuweza kumpa majukumu.
“Vilevile
tunamkaribisha Casillas nyumbani kama huko aliko anaona mambo hayaendi sawa,
hapa ni nyumbani na aliondoka kwa amani na tulimruhusu sisi wenyewe, hivyo
anakaribishwa,” alisema Kifaru.
0 COMMENTS:
Post a Comment