June 20, 2015

Matumaini ya Taifa Stars kushiriki michuano ya Chan yametoweka baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza nyumbani kwa kufungwa na Uganda kwa mabao 3-0.


Stars imepoteza mchezo huo leo kwenye Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar baada ya kuchapwa na wageni wake Uganda.

Wakati leo imepoteza, inasubiri kusafiri kwenda Uganda kuwavaa The Cranes, jambo ambalo linasubiri miujiza au aibu zaidi.

Wakati Stars imepoteza mechi hiyo, Kocha wake mkuu, Mart Nooij alitoka uwanjani hapo kama kiongozi wa serikali baada ya kusindikizwa na askari pamoja na mtu mmoja mwenye umbo kubwa anayeaminika ni mfanyakazi wa TFF.
Nooij amekuwa akipigiwa kelele na Watanzania ambao wanaonekana wamechoka na kufungwa kila kukicha.

Mholanzi huyo anaonekana wazi kuishindwa kazi yake, lakini TFF imekuwa inasita kumuondoa.

Hata hivyo, Watanzania wamekuwa wakipiga kelele kuhusiana na Mshauri wa Ufundi wa Rais wa TFF aitwaye Peregrinus Rutayuga ambaye anaonekana pia kuwa tatizo.


Wadau wamekuwa wakipiga kelele, Nooij, Rutayuga na memba wengine wa benchi hilo watupiwe virago.

1 COMMENTS:

  1. Kama tunataka matokeo mazuri , Timu ya Taifa Stars inatakiwa kuacha mara moja kucheza mpira kama wa Barca wa pasi fupi fupi manake hatuuwezi, wachezaji wetu hawana uwezo wa kumiliki mipira , pasi mbili tatu tu wameshapoteza mipira, hawajiamini na hawatulii wakiwa na mipira, mabeki hawajipangi vizuri wanapitwa ovyo, mabeki waige namna beki ya timu ya Taifa ya Italia inavyocheza ukimpita mmoja mwingine amefika. Kwasasa timu icheze pasi ndefu , mpira utoke nyuma na upigwe mbele si katikati manake hatwezi, viungo wapeleke mipira mbele kwa kulazimisha waache mara moja tabia ya kurudisha rudisha mipira nyuma na kujidai wanajua kupasiana sehemu ya kati kati ya uwanja na nyuma, timu ilazimishe kupeleka mbele mipira kwenye goli la adui , na walazimishe kupita na washambuliaji walete purukushani golini kwa adui si kuzembea na kuogopa kuumia manake ndo kazi walioichagua. Timu iache mara moja tabia ya kurudisha rudisha mipira nyuma na kujidai wanajipanga baada ya kushindwa kupita. Tunatakiwa kulazimisha mipira iende mbele na kulazimisha purukushani za kusaka mabao, tuache kujidai tunajua kujipanga tukiwa na mipira. Tunahitaji kuwapa washambuliaji wa pembeni idadi ya krosi wanazotakiwa kulazimisha kuzipiga golini na tunatakiwa kuwapa washambuliaji wa kati idadi ya mipira wanayotakiwa kupiga golini kwa adui na mechi inapoisha tufanye tathmini mawinga wamepiga krosi ngapi na washambuliaji wamepiga mipira mingapi golini, lazima tuwe na targets na hesabu bila hivyo ni kilio tu kila siku. Wachezaji wa Timu ya Taifa wanatakiwa kujua kuwa watanzania wanachukizwa sana na matokeo mabovu ya timu yao na tunajua kuwa wachezaji wetu hawajitumi kwa kiwango kinachotakiwa , hata aje Mourinho ni kazi bure kama morali ya wachezaji iko chini hatuwezi kufunga, wachezaji wetu wanatakiwa kujiamini na kupeleka mipira mingi golini kwa adui na si kujifanya wanajua kupigiana pasi nyingi zisizo na faida. Jambo la msingi pia ni kwa TFF na wadau wa mipira kuwajali wachezaji kwa kuwapa posho zao kwa wakati na tuchague viongozi wenye dhamira ya kweli ya kuendeleza soka Tanzania manake kuna viongozi wengi wako katika medani ya soka kimaslahi tu hawana faida na soka letu. Tunahitaji mipango endelevu ya kukuza vipaji vya watoto wanaocheza soka na tuwe tukiwapandisha kutoka timu za chini kwenda timu ya taifa. Kocha aache mara moja kuchagua wachezaji kwa majina nakumilikisha namba kwa baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa ambao kwa miaka mingi wamechezea timu ya taifa bila kuleta mafanikio yoyote, tuingize wachezaji wazuri wa timu ndogo na kuwatoa wachezaji wenye majina makubwa wa Simba na Yanga na Azam. Mwisho ninauliza swali , hivi haiwezekani kuitoa katika mashindano timu ya Taifa Stars? ni aibu tupu kwa taifa letu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic