Wakati wa usajili mabo
mengi yanatokea kwani nyota wa Simba, Emmanuel Okwi amebakisha miezi sita tu
kuitumikia timu yake na sasa anajadiliana na timu yake kuhusu kuongeza mkataba
baada ya Yanga kumwambia: “Noo, haiwezekani.”
Yanga wanadai Okwi baada
ya kuona yupo huru kuzungumza na timu yoyote kuhusu usajili wake, akaamua
kujaribu kwa kuzungumza na Wanajangwani lakini hawakuweza kufika mbali mapema
wakashindwana ndipo aliporudi Simba.
Okwi ambaye ametua Simba
msimu uliopita akiwa na mvutano na Yanga kwa utata wa kuvunja mkataba wake, kwa
sasa anajadiliana na viongozi wake ili kuongeza mkataba mapema kuepuka kuwa
mchezaji huru hapo baadaye.
Mmoja wa mabosi wa Kamati
ya Usajili ya Simba, amesema: “Okwi amebakiza mkataba wa
miezi sita, sasa tunafanya naye mazungumzo kwa ajili ya kuongeza mkataba
mwingine kabla ya huu wa awali kufikia tamati.”
“Mambo yakikaa vizuri
muda wowote kuanzia sasa Okwi atasaini mkataba mpya kwa mujibu wa makubaliano
na wala hakuna tatizo.”
Simba inaonekana
kujifunza kwa kosa lililofanywa na Yanga na Mbeya City kwa kuruhusu wachezaji
wake kujiunga na timu nyingine kama wachezaji huru baada ya kumaliza mikataba
yao.
Ngassa wa Yanga amejiunga
na Free State Stars ya Afrika Kusini kama mchezaji huru wakati Mbeya City imewaacha
Deus Kaseke akijiunga na Yanga na Peter Mwalyanzi akitua Simba wote wakiwa
wachezaji huru.
0 COMMENTS:
Post a Comment