Mwadui FC ya Shinyanga
haitaki mchezo na imesema tayari imemsajili beki wa kati David Mwantika
aliyemwagwa Azam FC, usibishe.
Awali, Mwantika alifanya mazungumzo na Simba mara mbili lakini wakaonekana kutopatana vizuri.
Timu hiyo iliyopanda
daraja na kupata tiketi ya kucheza msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kama ilivyo kwa
African Sports, Toto African na Majimaji, imetamba kwa usajili huo wa Mwantika
lazima itishe.
Mwenyekiti wa Mwadui ,
Omary Khatibu, aMEsema kila kitu kimeenda sawa na tayari wameshakamilisha
usajili wao kwa kumnasa Mwantika.
“Tumeshamalizana na
Mwantika ambaye tunaamini atatusaidia kwani ni chaguo la kocha wetu (Jamhuri
Kihwelo ‘Julio’),” alisema Khatibu.
Hadi sasa Mwadui imefanya
usajili wa baadhi ya wachezaji ambao ni Maregesi Mwanga na Rashid Mandawa
kutoka Kagera Sugar, Shaaban Kado (Coastal Union), Nizar Khalfan (Yanga),
Zahoro Pazi (Huru) Paul Nonga na Antony Matogolo kutoka Mbeya City.
“Kama mipango itabadilika
na kuwa na ulazima wa kusajili wachezaji wengine basi tutafanya hivyo lakini
kwa sasa tumemaliza kazi,” alisema Khatibu.
0 COMMENTS:
Post a Comment