![]() |
| HII NI JEZI YA SIMBA MSIMU ULIOPITA. |
Simba itavaa jezi mpya zenye muonekano wa aina yake ambazo ni "special order".
Jezi hizo zimetengenezwa na Kampuni kubwa ya vifaa vya Michezo ya Uhlsport.
Taarifa za uhakika zinaeleza jezi hizo zitawasili nchini siku chache zijazo na zimetengenezwa maalum kabisa kwa ajili ya Simba.
"Ni kweli, uongozi wa Simba ulitoa oda maalum. Halafu wataalamu wa ile kampuni wakatuma baadhi ya mifano ya jezi, zikachaguliwa na sasa ndiyo watatumia Simba," kilieleza chanzo.
Bado Simba haijaingia mkataba na kampuni hiyo lakini imekuwa ikihudumiwa vifaa na wadhamini wake Kilimanjaro.
Imeelezwa jezi hizo zitakuwa ni mara ya kwanza kuvaliwa na Simba na juhudi zinafanyika ili kuwe na maalum kwa ajili ya mashabiki.
Hata hivyo kumekuwa na siri kubwa kuhusiana na kuzianika mapema wakihofia wezi wa kudurufu.








0 COMMENTS:
Post a Comment