Timu ya African Sports ya Tanga, imeamua kufanya kweli baada ya
kupania kumnasa straika wa Yanga, Hussein Javu, kwa nguvu yoyote ile kwa ajili
ya kuwasaidia kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Benchi la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Kocha Mkuu, Mrage
Kabange, liameamua kumpitisha Javu baada ya mchujo wa listi ndefu ya mastraika
waliyokuwa nayo mkononi.
Lakini imefafanuliwa kuwa awali waliingia hofu ya kupeleka maombi
yao hayo Yanga baada ya kusikia fununu za Javu kuhitajika na Majimaji ya Songea
na pia mipango ya kupelekwa kwa mkopo Stand United.
Mtu wa ndani wa Sports amelijuza gazeti hili: “Kwa sasa hapa
anatafutwa straika na kiungo wa kati, kwenye straika karata imedondoka kwa
Javu, kocha ameuagiza uongozi ufanye juu chini kuhakikisha unamnasa kwa kuwa
anaamini ni mshambuliaji atakayechangia mafanikio msimu ujao, kwa hiyo harakati
zimeshaanza.”
Alipotafutwa Kabange kuizungumzia ishu hiyo, alisema: “Ninachoweza
kusema ni kwamba usajili bado unaendelea na bado tupo mawindoni tunaangalia
nafasi za wachezaji tunaowataka na wengine tunazungumza nao na kama kutakuwa na
chochote basi muda ukifika tutaweka wazi,” alisema Kabange.







0 COMMENTS:
Post a Comment