Kikosi kizima cha APR kinatarajia kutua
nchini kesho saa 4 usiku tayari kwa michuano ya Kombe la Kagame.
Michuano ya Kagame inatarajia kuanza
nchini Jumamosi na itafanyika katika viwanja vya Taifa na Karume jijini Dar es
Salaam.
Uongozi wa APR umethibitisha kikosi chao
kuwa kitawasili saa 4 usiku.
APR ni kati ya timu ambazo zimekuwa
zikitoa ushindani mkubwa katika michuano hiyo ambayo inadhaminiwa na shabiki
wake namba moja, Rais wa Rwanda, Paul Kagame.
0 COMMENTS:
Post a Comment